MAREKANI-CHANJO-COVID 19

Coronavirus: Chanjo kuanza kutolewa ndani ya saa 24 zijazo nchini Marekani

Chanjo iliyotengezwa na kampuni ya Pfizer na BioNTech
Chanjo iliyotengezwa na kampuni ya Pfizer na BioNTech JOEL SAGET / AFP

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa chanjo ya kwanza ya COVID-19 nchini Marekani itaanza kutolewa katika muda wa saa ishirini na nne zijazo.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka ya kukagua Chakula na Dawa Marekani, FDA, ilitoa idhini ya matumizi ya dharura ya chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na maambara ya Pfizer na BioNTech.

FDA inatarajiwa kuidhinisha ifikapo Jumapili chanjo mpya ya kupambana na virusi vya corona.

Maafisa wengi wa Marekani wanasubiri idhini ya chanjo baada ya mkutano wa Desemba 10, ingawa afisa wa FDA hivi karibuni alisema uamuzi kama huo unaweza kuchukua wiki kadhaa.

Donald Trump, ambaye aliweka shinikizo kwa maabara, anaweza kurekodi ushindi wa mwisho pamoja na uuzaji wa chanjo hiyo wiki chache kabla ya kumkabidhi madaraka mrithi wake Joe Biden.