BRAZIL-COVID 19

Coronavirus: Vifo 180,000 vyathibitishwa Brazil

Wagonjwa wa janga la Corona nchini Brazil
Wagonjwa wa janga la Corona nchini Brazil AFP / MICHAEL DANTAS

Brazil imepitisha kizingiti cha vifo 180,000 kutokana virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19, na kusababisha raia wengi kuwa na hofu ya kuongezeka kwa vifo, ikiwa serikali haitachukuwa hatua kali.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya afya imeripoti vifo vipya 646 katika muda wa saa 24 zilizopita, na kusababisha jumla ya vifo 180,411.

Idadi ya visa vipya vya maambukizi imefikia 53,030, kwa jumla ya visa 6,834,829 nchini.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.