MAREKANI-COVID 19

Covid 19: Zaidi ya kesi mpya 240,000 na vifo 3,000 vyathibitishwa nchini Marekani

Kwa mara ya kwanza tangu katikati ya mwezi Agosti, zaidi ya vifo 1,400 vimerekodiwa (1,450), wakati idadi ya wagonjwa hospitalini iliendelea kuongezeka haraka nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza tangu katikati ya mwezi Agosti, zaidi ya vifo 1,400 vimerekodiwa (1,450), wakati idadi ya wagonjwa hospitalini iliendelea kuongezeka haraka nchini Marekani. REUTERS

Vituo vya Marekani vya Kudhibiti na Kuzuia Magonjwa (CDC) Jumamosi vimeripoti visa 244,011 zaidi kuliko siku moja kabla na vifo vipya 3,013, na kusababisha idadi ya fifo kufikia 294,535 kwa jumla ya visa 15,718,811 vya maambukizi .

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Ijumaa rais wa Marekani Donald Trump alitangaza kuwa chanjo ya kwanza ya COVID-19 nchini Marekani itaanza kutolewa hivi punde.

Mamlaka ya kukagua Chakula na Dawa Marekani, FDA, ilitoa idhini ya matumizi ya dharura ya chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na maambara ya Pfizer na BioNTech.

FDA inatarajiwa kuidhinisha leo Jumapili chanjo mpya ya kupambana na virusi vya Corona.

Afisa wa FDA hivi karibuni alisema uamuzi kama huo unaweza kuchukua wiki kadhaa.

Donald Trump, ambaye aliweka shinikizo kwa maabara, anaweza kurekodi ushindi wa mwisho pamoja na uuzaji wa chanjo hiyo wiki chache kabla ya kumkabidhi madaraka mrithi wake Joe Biden.