MAREKANI

Marekani: Mpango wa dola Bilioni 908 kuwasilishwa rasmi na Wabunge Jumatatu

Spikq wa bunge la Marekani, Nancy Pelosi.
Spikq wa bunge la Marekani, Nancy Pelosi. REUTERS/Jonathan Ernst

Kundi la wabunge kutoka vyama vya Republican na Democrat katika Bunge la Congress wanatarajia kuwasilisha rasmi leo Jumatatu nakala inayoeleza mpango wa kusaidia uchumi wa Marekani wa dola Bilioni 908 (sawa na euro Bilioni 754).

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na mtu aliyekaribu na faili hii, pendekezo la mpango huo litagawanywa katika vifurushi viwili tofauti vya bajeti kwa matumaini ya kushawishi mabunge yote mawili.

Sehemu ya mpango wa kiasi cha dola bilioni 748 itawekwa katika mpango wa misaada wa makampuni madogomadogo na wasio na ajira na pia ufadhili wa utoaji wa chanjo za COVID-19, chanzo hicho kimesema. Kipengele kingine kitahusu hasa hoja za mzozo kati ya Republican na Democrats: ulinzi wa makampuni na fedha kwa jamii na tawala za mitaa.

Mmoja wa maseneta kutoka chama cha Democrat, walio karibu na fali hiyo Joe Manchin anasema, nakala hiyo itawasilishwa rasmi leo Jumatatu.

Wabunge wa vyama vya Republican na Democrats wamekuwa wakijaribu kwa miezi kadhaa kufikia makubaliano juu ya mpango wa tatu.