CANADA

Covid-19: Canada yazindua kampeni yake ya chanjo

Raia kwenye mji wa Montréal, Canada wakiendelea kuchukua tahadhari
Raia kwenye mji wa Montréal, Canada wakiendelea kuchukua tahadhari REUTERS/Christinne Muschi/File Photo

Canada imezindua kampeni kubwa ya chanjo dhidi ya Covid-19 katika miji ya Quebec , Montreal na Toronto chini ya wiki moja baada ya kuidhinishwa chanjo ya Pfizer-BioNTech na mamlaka ya Canada.

Matangazo ya kibiashara

Kuzinduliwa rasmi kwa kampeni hii, ambayo haijawahi kufanyika nchini Canada tangu vita vya pili vya dunia, ni "kazi kubwa," Waziri Mkuu Justin Trudeau amesema katika mahojiano na Radio-Canada.

Runinga ya taifa imerusha moja kwa moja zoezi la kwanza la chanjo hiyo karibu saa 12 jioni kutoka hospitali ya huko Toronto.

Saa moja baadaye, Waziri wa Afya wa Quebec alitangaza kwamba Gisèle Lévesque, mwanamke mwenye umri wa miaka 89, alipewa chanjo muda mfupi baada ya saa 11:30 mchana jana Jumatatu katika kituo cha kuwahudumia wazee katika mji wa Quebec.