MAREKANI

Marekani: Ushindi wa Biden washibitishwa, Trump aendelea kudai udanganyifu

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden akiteta jambo na naibu wake Kamala Haris
Rais mteule wa Marekani, Joe Biden akiteta jambo na naibu wake Kamala Haris REUTERS/Mike Blake

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amethibitishwa rasmi na Jopo la wajumbe maalumu lenye nguvu ya kumchagua rais wa Marekani, maarufu kama Electoral College, kuwa rais wa taifa hilo.

Matangazo ya kibiashara

Kulingana na jopo hilo alishinda kwa kura 306 dhidi ya 232 alizopata Donald Trump. Matokeo yatatangazwa Januari 6 katika Bunge la Congress, hata kama rais anayemaliza muda wake bado anakataa kutambua ushindi wa mpinzani wake.

 

Katika hotuba aliyoitoa baada ya kutangazwa kwa ushindi huo , alisema kuwa demokrasia ya Marekani ''imesukumwa na kujaribiwa '' na "imedhihirisha kuwa ni jasiri, ya kweli na thabiti ''.

 

Bw Biden pia amezungumzia kuhusu hatua ya Trump ya kujaribu kupinga matokeo ya uchaguzi.

 

'Utashi wa watu umeshinda ' amesema Joe Biden baada ya ushindi wake kuthibitishwa.

 

Bw Biden alisema kuwa ni muda wa "kugeuza ukurasa, kama ambavyo tumekuwa tukifanya katika kipindi chote cha historia -kuungana na kupona".