MAREKANI-COVID19

Marekani yarekodi idadi ya juu zaidi ya maambukizi ya Covid 19

Mfano wa sindano ambayo hutumika kuchoma chanjo
Mfano wa sindano ambayo hutumika kuchoma chanjo Reuters/Lindsey Wasson

Zaidi ya watu 300,000 wamefariki dunia kutokana na ugonjwa hatari waCOVID-19 nchini Marekani, kulingana na takwimu zilizotolewa na kituo cha kuzuia na kudhibiti magonjwa cha Johns Hopkins

Matangazo ya kibiashara

Taifa hili linaloongoza kiuchumi duniani linaendelea kurekodi vifo na maambukizi zaidi, na kupitisha mara kwa mara visa vya kila siku 200,000 na vifo 2,500, au hata 3,000, kwa siku.

 

Hayo yabnajiri wakati chanjo ya virusi vya corona iliyotengenezwa na kampuni mbili za Pfizer na BioNTech ilianza kutolewa kwa mara ya kwanza leo Jumatatu Desemba 14, siku kadhaa tangu matumizi yake yalipoidhinishwa, kulingana na maafisa aw Marekani.

Katika awamu hiyo ya kwanza watu milioni 3 watapatiwa chanjo, huku watumishi wa afya na wahudumu walio mstari wa mbele watapewa kipaumbele katika utoaji wa chanjo dhidi ya virusi vya Corona.

Zoezi la utoaji chanjo litaanza kwa asilimia 100, kwa mujibu wa Jenerali wa Jeshi la Marekani anayesimamia usambazaji wa chanjo hiyo, Gus Perna, wakati dozi za kwanza zilisafirishwa juzi Jumapili.

Kampuni ya Pfizer imesema kiasi dozi milioni 25 zinaweza kuwa tayari kwa ajili ya kutimika nchini Marekani ifikapo mwishoni mwa mwezi Disemba. Hivi sasa nchi hiyo imeagiza dozi milioni 100.

Kampuni inayotengeneza chanjo hiyo imesema inafanya kazi na washirika wengine kuanza kusafirisha chanjo kwa kutumia magari ya mizigo kutoka kwenye maghala yake yaliyoko kwenye majimbo Michigan na Wisconsin  kwenda majimbo yote 50 ya Marekani.