MAREKANI

Mwanasheria mkuu wa Marekani atangaza kujiuzulu

Rais wa Marekani, Donald Trump akiwa na mwanasheria wake mkuu William Barr.
Rais wa Marekani, Donald Trump akiwa na mwanasheria wake mkuu William Barr. REUTERS/Leah Millis

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza kuwa Mwanasheria Mkuu wa Serikali William Barr ataondoka madarakani kabla ya Krismasi na naibu wake Jeff Rosen atachukua wadhifa huo wa muda.

Matangazo ya kibiashara

Katika barua kwa Donald Trump ambayo shirika la habari la REUTERS linasaema limepata, William Barr ametangaza kwamba ataondoka madarakani mnamo Desemba 23.

 

Katika barua yake, William Barr alisifu kile alichokiita rekodi ya kihistoria ya kampeni ya Trump, akisema imesaidia kukuza uchumi, kuimarisha jeshi na kuzuia uhamiaji haramu .

 

"Ninajivunia kuchangia katika sehemu ya mafanikio mengi na kazi kubwa ambayo ulifanya kwa maslahi ya taifa la Marekani na wananchi wake," ameandika William Barr.

 

Hatima ya William Barr katika siku za mwisho za utawala wa Trump imekuwa ilikuwa matatani tangu aliposema mapema mwezi huu kwamba uchunguzi wa wizara ya Sheria haupata udanganyifu wowote wa kura kuhusiana na uchaguzi wa urais, uchunguzi ambao ulipingana na tuhuma za Donald Trump ambazo hazina msingi wowote.