MAREKANI-JOE BIDEN

Marekani: Biden arejea kwenye kampeni za uchaguzi wa maseneta

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden.
Rais mteule wa Marekani, Joe Biden. Angela Weiss / AFP

Siku moja baada ya ushindi wake kuthibitishwa na Jopo la wajumbe maalumu lenye nguvu ya kumchagua rais wa Marekani, maarufu kama Electoral College, Rais mteule wa Marekani amesafiri kwenda Georgia kwa uchaguzi wa maseneta Januari 5.

Matangazo ya kibiashara

Viti viwili vinapaswa kujazwa na Chama cha Democratic kinataka kupata ushindi wa viti vyote viwili ili kupata idadi kubwa ya maseneta katika Baraza la Bunge.

"Tuna uwezo wa kufafanua ukurasa ujao katika historia ya Marekani," amesema Jon Ossof, mmoja wa wagombea wawili wa chama cha Democratic kutoka Jimbo la Georgia katika uchaguzi wa maseneti uliopangwa kufanyika Januari 5, 2021.

Kama ishara ya umuhimu wa uchaguzi huu, baada ya hotuba yake, mgombea alitoa nafasi kwa rais mteule Joe Biden, ambaye alikuja kuwaunga mkono katika uchaguzi huo, akiwa na ujumbe kama huo.

“Mlipiga kura kwa idadi kubwa na mlipiga kura kana kwa namana mlivyojiamini. Januari 5, bado mtalazimika kupiga kura kwa idadi kubwa! Na hii ndio inatakikana. Nadhani Georgia itashangaza wengi kwa idadi ya watu watakaopiga kura Januari 5, ”amesema Joe Biden huku akipongezwa kwa makofi na honi.

Rais mteule amewasifu wagombea hao wawili: "Wanataka kuwatumikia raia wa Georgia na sio masilahi yao," amesema.

Ili kushinda, Wademocrats wanapaswa kufaulu kuhamasisha wapiga kura wote katika jimbo la Georgia ambao walikwenda kupiga kura mnamo mwezi Novemba kumaliza muhula wa Donald Trump.