MAREKANI

Covid-19: Zaidi ya vifo 3,700 vyathibitishwa Marekani

Kwa mara ya kwanza tangu katikati ya mwezi Agosti, zaidi ya vifo 1,400 vimerekodiwa (1,450), wakati idadi ya wagonjwa hospitalini iliendelea kuongezeka haraka nchini Marekani.
Kwa mara ya kwanza tangu katikati ya mwezi Agosti, zaidi ya vifo 1,400 vimerekodiwa (1,450), wakati idadi ya wagonjwa hospitalini iliendelea kuongezeka haraka nchini Marekani. REUTERS

Marekani imeendelea kurekodi ongezeko la visa  vingi vya maambukizi pamoja na vifo vinavyotokana na ugonjwa hatari wa COVID-19.

Matangazo ya kibiashara

Siku ya Jumatano pekee Marekani ilirekodi idadi kubwa ya zaidi ya watu 3,700 waliofariki dunia na visa vipya 250,000 vya maambukizi ya virusi vya Corona kwa siku moja, rekodi ambayo ni mara mbili tangu kuzuka kwa janga hilo nchini humo, kulingana na takwimu kutoka Chuo Kikuu cha Johns Hopkins.

 

Marekani inaendelea kukabiliwa na ongezeko la maambukizi ya virusi vya Corona vinavyosababisha ugonjwa hatari wa COVID-19 kwa zaidi ya mwezi mmoja.

 

Baadhi ya watu 113,000 pia wamelazwa hospitalini kwa sababu ya virusi hivyo, kulingana na takwimu kutoka wizara ya Afya ya Marekani. Hii pia ni idadi kubwa.