MAREKANI-COVID19

Marekani yaelekea kuidhinisha chanjo ya pili ya Corona

Chanjo ya Moderna, ambayo Marekani inaelekea kuiidhinisha.
Chanjo ya Moderna, ambayo Marekani inaelekea kuiidhinisha. Photo AP / Hans Pennink

Timu ya wataalamu nchini Marekani, imepiga kura kupendekeza kuidhinishwa kwa chanjo ya pili ya kukabiliana na virusi vya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Maofisa kutoka mamlaka ya dawa na chakula nchini humo, FDA, wanatarajiwa kufuata mapendekezo ya wataalamu hao, hatua inayomaanisha kuwa chanjo ya Moderna huenda ikaanza kutolewa kuanzia juma lijalo.

Kura hii imekuja ikiwa ni siku chache tu kupita tangu taifa hilo liidhinishe matumizi ya chanjo nyingine ya faiza BioTech, wakati huu ikirekodi idade ya juu ya maambukizi na vifo kuliko taifa lolote lile duniani.

Watengenezaji wa chanjo ya Moderna, wamesema juma hili kuwa dawa yao iko salama kwa matumizi kwa zaidi ya asilimia 94.

Marekani imekubali kununua zaidi ya dozi milioni 200 na kwamba dozi milioni 6 ziko tayari kuanza kusambazwa ikiwa mamlaka ya chakula na dawa itaidhinisha matumizi yake.