ISRAEL-MAREKANI

Israel kurejesha uhusiano na nchi ya tano ya Kiiislamu kabla ya Trump kuondoka

Rais wa Marekani, Donald Trump.
Rais wa Marekani, Donald Trump. MANDEL NGAN AFP

Israel imejikita kwa kina kuhalalisha uhusiano na nchi ya tano ya Kiiislamu katika bara la Asia kabla rais wa Merika Donald Trump kukabidhi madaraka kwa mrithi wake Joe Biden ndani ya kipindi kisichozidi mwezi mmoja, waziri wa Israeli amesema Jumatano.

Matangazo ya kibiashara

Ikulu ya White House tangu mwezi Septemba imefaulu kurejesha uhusiano wa kidiplomasia kati ya Israel na nchi nne za Kiislamu, Falme za Kiarabu, Bahrain, Sudan na Morocco.

 

Alipoulizwa na tovuti ya habari ya Ynet TV juu ya kuingizwa kwa nchi ya tano kwenye orodha kabla ya Donald Trump kuondoka White House Januari 20, Waziri wa Ushirikiano wa Kikanda wa Israeli Ofir Akunis amejibu: " Tunafanya kazi katika mwelekeo huo. "

 

"Ninaamini (...) kwamba kutakuwa na tangazo kutoka Marekani juu ya nchi nyingine iliyo tayari kurejesha uhusiano wake na Israeli na, kufikia mkataba wa amani, ” Ofir Akunis ameongeza.

 

Tunisia ilisema Jumanne kwamba haiko tayari kurejesha uhusiano wake na serikali ya Kiyahudi.

 

Kulingana na Ofir Akunis, kuna nchi mbili kuu ambazo zinataka kurejesha uhusiano wao na Israel. Moja, inapatikana Ghuba, inaweza kuwa Oman lakini sio Saudi Arabia wakati nyingine, inayopatikana mashariki, ni "nchi ya Kiislamu ambayo inasadikiwa kuwa ni Pakistan.

 

Indonesia, nchi yenye Waislamu wengi zaidi, ilitangaza wiki iliyopita kwamba haitatambua Israeli hadi mahitaji ya serikali ya Palestina yatimizwe, sera inayoigwa na jirani yake wa Asia Kusini, Malaysia.

 

Huko Dhaka, afisa wa wizara ya mambo ya nje amesema Bangladesh pia haina nia ya kuanzisha uhusiano wa kidiplomasia na Israeli.

 

Wakati mazungumzo ya Israeli na Palestina, yaliyoanza zaidi ya robo ya karne iliyopita, yamekwama tangu mwaka 2014, Wapalestina wanahofia kuwa watawekwa kando na mchakato huu wa kurejeshwa kwa uhusiano kati ya nchi za Kiislamu na Israel.