MEXICO

Idadi ya vifo yaongezeka Mexico na kufikia zaidi ya 120,000 kutokana na Covid 19

Wahudumu wa afya wanaopambana na janga la Covid 19
Wahudumu wa afya wanaopambana na janga la Covid 19 AP Photo/Pavel Golovkin

Mexico imerekodi visa vipya 11,653 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo vipya 816 kutokana na ugonjwa huo katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, wizara ya afya imetangaza.

Matangazo ya kibiashara

Kufikia sasa Mexico ina wagonjwa 1,350,079 walioambukizwa virusi vya Corona na vifo 120,311, kulingana na takwimu rasmi.

Mamlaka nchini humo ilionya kuwa idadi halisi ya watu walioambukizwa virusi vya Corona huenda ikazidi idadi ya visa vilivyorekodiwa.

Mlipuko wa virusi vya corona unaosababisha ugonjwa wa COVID-19, ulitokea katika mkoa wa Hubei nchini China mwishoni mwa mwaka 2019.

Kufikia sasa kinachojulikana ni kuwa COVID-19, ni ugonjwa ambao unaothiri mfumo wa kupumua wa binadamu.

Dalili zake ni pamoja na homa kali, kukohoa ambako baada ya wiki moja muathiriwa anakabiliwa na tatizo la kupumua.