MAREKANI

Trump awasamehe washirika wake wa karibu wa zamani kabla ya kukabidhi madaraka

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump (AP / JPP)

Rais wa Marekani Donald Trump ametangaza msamaha kwa aliyekuwa Meneja wa Kampeni yake Paul Manafort, aliyekuwa mshauri wake Roger Stone na mkwe wake Charles Kushner.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya pili kwa rais Trump anayeondoka madarakani kutoa msamaha huo ndani ya siku mbili kwa washirika wake wa karibu, na ametoa tangazo hili baada ya kuwasili katika jimbo la Florida kwa mapumziko ya Krismasi.

Hadi sasa Trump ametangaza msamaha kwa watu 26 kuelekea kumalizika kwa muhula wake tarehe 20 mwezi Januari mwaka 2021 wakati rais mteule Joe Biden atakapoapishwa.

Miongoni mwa watu mashuhuri ambao wamesamehewa na rais Trump ni Robert Mueller aliyekuwa Mkuu wa FBI aliyekuwa anachunguza madai ya Urusi kuingilia uchaguzi wa Marekani mwaka 2016, na kumsaidia Trump kushinda.

Bahati hiyo ameipata pia aliyekuwa mshauri wa kitaifa wa masuala ya usalama Michael Flynn pamoja na aliyekuwa mshauri wake Roger Stone aliyekuwa amepatikana na hatua ya kulidanganya bunge.

Marais nchini Marekani wamekuwa na utaratibu wa kutanangaza msamaha kwa watu mbalimbali kabla ya kuondoka madarakani kwa mujibu wa katiba ya nchi hiyo.