UFILIPINO

Ufilipino yakumbwa na tetemeko la ardhi lenye nguvu ya 6.3

Tetemeko la ardhi lenye ukubwa wa 6.3 limepiga nchini Ufilipino leo Ijumaa, kulingana na Idara ya Jiolojia ya Marekani (USGS), likitikisa majengo na kukatiza ibada za Krismasi, lakini bila kusababisha majeruhi au uharibifu wowote.

Tetemeko la ardhi
Tetemeko la ardhi Reuters/路透社
Matangazo ya kibiashara

Tetemeko hilo la ardhi limetokea katika mkoa wa Batangas katika kisiwa kikuu cha Luzon saa 7:43 asubuhi (sawa na saa 5:43 usiku saa za kimataifa), kulingana na USGS. Kina cha tetemeko la ardhi (kilomita 114) hufanya uwezekano wa kuwepo na wahanga au uharibifu mkubwa wa majengo, kulingana na Idara ya Jiolojia ya Marekani (USGS).

Hata hivyo, mashahidi, wanasema kwamba majengo katika mji mkuu Manila yametikisika na ibada za Krismasi zimesitishwa. "Misa nyingi zimesitishwa kwa muda wa kutosha kutokana na tetemeko hilo  lakini waumini hawakuogopa," amesema Carlo Caceres, mkuu wa polisi wa Calatagan, mji ulio karibu na kitovu cha tetemeko la ardhi kilomita 90 kusini mwa Manila.

"Mara nyingi hutokea matetemeko ya ardhi katika eneo hilo na watu wamezoea," ameongeza.