MAREKANI-CHINA

Washington yaimarisha agizo juu ya uwekezaji katika makampuni ya Wachina

Donald Trump, Novemba 20, 2020.
Donald Trump, Novemba 20, 2020. MANDEL NGAN AFP

Utawala wa Trump umeimarisha agizo la linalopiga marufuku uwekezaji wa Marekani katika makampuni ambayo Washington inaamini yanamilikiwa au kudhibitiwa na jeshi la China.

Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Fedha ya Marekani imetoa muongozo wa kuweka wazi hatua hizo, ikisema zitatumika kwa fedha za viwango zilizoorodheshwa (ETFs) na pia makampuni tanzu za China zinazoaminika kumilikiwa au kudhibitiwa na jeshi la China.

Kulingana na chanzo rasmi katika faili hiyo, Idara ya wizara Mambo ya Jje na wizara ya Ulinzi wamepinga zimetofautiana kuhusu hatua hiyo wizara ya Fedha ya kulegeza vifungo vya agizo hilo.

Siku ya Jumatatu waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani alisema kwamba tangazo hilo "linahakikisha kuwa mitaji ya Marekani haichangii katika maendeleo na uboreshaji wa jeshi la China, ujasusi na idara za usalama".

"Hii ni lazima iondoe hofu kwamba wawekezaji wa Marekani wanaweza kusaidia bila kujua (kampuni zinazodhibitiwa na jeshi la China) moja kwa moja, kwa njia isiyo ya moja kwa moja au kupitia uwekezaji mwingine tu," Pompeo aliongeza.

Vyombo vya habari kadhaa vimeripoti kwamba wizara ya Fedha inatafuta hasa kuyaondoa makampuni tanzu ya makampuni ya China yaliyowekwa kwenye "orodha nyeusi" iliyotangazwa na Ikulu ya White House.