AUSTRALIA

Hatua zaimarishwa Sydney kabla ya Mwaka mpya kudhibiti Covid 19

Abiria wakiwa katika uwanja wa ndege jijini Sydney
Abiria wakiwa katika uwanja wa ndege jijini Sydney PETER PARKS / AFP

Mamlaka nchini Australia imeongeza hatua za kukabiliana na kusambaa kwa virusi vya Corona kabla ya Mwaka Mpya. Miongoni mwa hatua zilizoongezwa ni pamoja na marufuku ya watu kutembea marufuku ya mikusanyiko katika mji mkuu wa Sydney.

Matangazo ya kibiashara

Mamlaka inaona kwamba pamoja na hatua hizi wana imani kuwa  ni njia moja wapo ya kuzuia "kuenea haraka" kwa virusi vya Corona wakati wa sherehe za Mwaka Mpya, wakati aina mpya ya virusi vya Corona imegunduliwa hivi karibuni nchini Uingereza.

Idadi ya watu katika mikusanyiko ya watu binafsi imepuguzwa hadi watu watano, wakati kizingiti cha juu cha mikusanyiko ya nje ya umma kimepunguzwa hadi watu 30. Makazi ya matibabu ni marufuku kwa wageni.

Mamlaka pia imetenga eneo linalojulikana kama "eneo maalumu" pembezoni mwa bandari, ambapo fataki za jadi hupigwa kila mwaka.

Wakazi tu wa eneo hilo na watu ambao wameomba na kupata idhini, pamoja na cheti cha matibabu, wataweza kwenda katika eneo hilo usiku wa kuamkia Mwaka Mpya.

Australia imefanikiwa kupunguza visa 28,300 vya maambukizi tangu kuzuka kwa janga hilo , wakati jumla ya vifo 909 vimerekodiwa.