MAREKANI

Kisa cha kwanza aina mpya ya virusi vya Corona charipotiwa Marekani

Kirusi kipya cha corona
Kirusi kipya cha corona NIAID-RML via AP

Marekani imerekodi kisa cha kwanza cha aina mpya ya kirusi cha Corona kinachoaminka kusambaa kwa kasi, kilichoanzia nchini Uingereza.

Matangazo ya kibiashara

Kisa hiki kimeripotiwa katika jimbo la Colorado Jumanne wiki hii. Kirusi hicho kimegundulika kwa kijana wa miaka 20 ambaye hana historia ya kusafri

Rais mteule wa Marekani Joe Biden ameonya kwamba hali mbaya ya Covid-19 inaweza isiwe rahisi hadi kufikia mwezi Machi.

Aidha Biden ameongeza kuwa changamoto iliyopo ni kampeni kubwa ya utoaji chanjo huko akiukosoa mpango wa mtangulizi wake Donald Trump katika usambazaji chanjo. Hata hivyo Joe Biden ameapa kuzidisha juhudi za utoaji wa chanjo.

 Wakati huo huo serikali ya Uingereza imekuwa chini ya shinikizo la kuzidisha vizuizi wakati rekodi ya maambukizi mapya ikifikia 53,135 ndani ya saa 24.

Ufaransa inakusudia kuanza marufuku ya usiku mapema jioni katika baadhi ya maeneo ya nchi.

Waziri mwenye dhamana ya afya Olivier Veran, amesema hata hivyo serikali haitofunga shughuli za umma. Ufaransa hadi sasa imesajili visa milioni mbili na nusu na vifo nchini humo ni elfu 64,000