MAREKANI

Washington yatangaza ushuru wa ziada kwa bidhaa za Ufaransa na Ujerumani

Rais wa Marekani, Donald Trump.
Rais wa Marekani, Donald Trump. AP Photo/Julio Cortez

Marekani imetangaza kuwa itaweka ushuru wa ziada kwa bidhaa kutoka Ufaransa na Ujerumani, kulipiza kisasi kwa ushuru uliowekwa na Jumuiya ya Ulaya kwa bidhaa kutoka nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Marekani inaona kuwa ushuru uliowekwa kwa bidhaa kutoka nchini humo unapindukia na sio halali kutokana na wigo uliochaguliwa kwa kuhesabu.

Bidhaa muhimu kutoka Ufaransa na Ujerumani vitatozwa ushuru kwa kulipiza kisasi, na vitaongezwa kwenye orodha ya bidhaa vinavyotozwa ushuru tangu mwaka 2019, kulingana na taarifa kutoka Mwakilishi wa Biashara wa Marekani (USTR).

Ushuru huu wa forodha ni sehemu ya mzozo juu ya misaada ya umma inayolipwa kwa makampuni ya Airbus na Boeing.

Umoja wa Ulaya pia uliruhusiwa mwaka huu na Shirika la Biashara Ulimwenguni (WTO) kutoza ushuru wa ziada wa forodha kwa bidhaa kutoka Marekani.

Lakini Washington inaamini kuwa imeadhibiwa kwa mfumo wa hesabu  uliyochaguliwa, ambao, kulingana na utawala wa Trump, umesababisha kiwango cha
juu sana cha ushuru wa forodha unaotozwa kwa bidhaa kutoka Marekani.