MAREKANI

Donald Trump atoa wito kwa Georgia kusimama 'kuokoa Marekani'

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump MANDEL NGAN / AFP

Usiku wa kuamkia uchaguzi muhimu nchini Marekani, rais anayemaliza muda wake alifanya mkutano saa chache zilizopita huko Georgia.

Matangazo ya kibiashara

Donald Trump alikuja kuwaunga mkono maseneta wawili kutoka chama cha Republican wanaomaliza muda wao ambao wanawania nafasi zao katika Bunge la Seneti Jumanne hii, Januari 5.

Uchaguzi ambao unatarajia kuamua ni chama gani kati ya Republican na Democratic kitaibuka na viti vingi katika Bunge la Seneti.

Wakati huo huo rais Donald Trump kwa mara nyingine alitumia fursa hiyo kupinga kuwa alishindwa katika ucahuguzi wa urais uliyofanyika mapema mwezi Desemba 2020.

Donald Trump anaendelea na msimamo wake wa kupinga matokeo ya uchaguzi yaliyompa ushindi mpinzani wake kutoka chama cha Democratic, Joe Biden.

"Nilishinda Georgia", "hatuwezi kupoteza Georgia", "huu ni uchaguzi uliogubikwa na udanganyifu mkubwa". Haya ni maneno yake ya kwanza Jumatatu hii jioni alipofika jukwaani.

Hata hivyo, matokeo ya kura yalihesabiwa mara kadhaa huko Georgia na ni wazi:  Joe Biden ndiye ambaye alishinda uchaguzi wa urais na ndiye ambaye alishinda katika jimbo hili kwa kura 12,000 dhidi ya Donald Trump.

Siku ya Jumatatu hii jioni, Donald Trump alimshambulia gavana wa jimbo la Georgia, ambaye ni mmoja wa wafuasi wake wa zamani na kamishna wa uchaguzi katika jimbo la Georgia Brad Raffensperger, ambaye anamshinikiza kubadili matokeo.

"Watu wasio na uwezo", amemshutumu Trump. Katika hotuba yake yote, rais aliendelea kutoa habari za uwongo, akibaini kwamba uchaguzi uligubikwa na udanganyifu mkubwa, na kusema kulikuwepo na wapiga kura hewa.