MEXICO-COVID 19

Mexico yaidhinisha chanjo dhidi ya Corona ya AstraZeneca

Chanjo ya AstraZeneca
Chanjo ya AstraZeneca REUTERS

Mamlaka ya dawa nchini Mexico ameidhinisha utumiaji wa dharura wa chanjo ya COVID-19 iliyotengenezwa na maabara ya AstraZeneca na Chuo Kikuu cha Oxford, waziri wa mambo ya nje wa Mexico ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

"Uzalishaji utaanza hivi karibuni nchini Mexico," Marcelo Ebrard amesema kwenye Twitter, akikaribisha "habari njema ".

Kwa hivyo Mexico inaungana na Uingereza, nchi ya kwanza duniani kutoa idhini ya matumizi ya chanjo hii, Desemba 30, 2020.

Chanjo ya Oxford-AstraZeneca iliidhinishwa kwa matumizi nchini Uingereza, na dozi ya kwanza ilianza kutolewa Jumatatu wiki hii wakati ambapo visa vya virusi vya Corona vinaendelea kuongezeka.

Hivi karibuni Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson alitaja maendeleo ya chanjo hiyo "ushindi mkubwa" kwa sayansi Uingereza, na kuongeza kuwa: "Sasa tutaanza kutoa chanjo hii kwa wengi haraka iwezekanavyo."

Pia utolewaji wa chanjo hiyo unatarajiwa kuwa wa juu zaidi wakati huu ambapo dunia inakabiliana na virusi vya corona hasa ukizingatia kuwa ni rahisi kuihifadhiwa na kuitengeneza kwa kiwango cha juu ikilinganishwa na chanjo nyingine.