MAREKANI

George W. Bush kuhudhuria hafla ya kuapishwa Joe Biden

Marais wa zamani wa Marekani  Barack Obama (Kushoto) na George W. Bush (Kulia) wakati wa kumwapisha Donald Trump mwaka 2019
Marais wa zamani wa Marekani Barack Obama (Kushoto) na George W. Bush (Kulia) wakati wa kumwapisha Donald Trump mwaka 2019 REUTERS/Kevin Lamarque/Files

Rais wa zamani wa Marekani George W. Bush amepanga kuhudhuria sherehe za kuapishwa kwa rais mteule wa Marekani Joe Biden kutoka chama cha Democratic Januari 20, amesema msemaji wa George W. Bush, rais wa zamani kutoka chama cha Republican.

Matangazo ya kibiashara

"Rais na Bi Bush wanatarajia kwenda Capitol Hill kwa ajili ya kuapishwa kwa rais Biden na Makamu wa rais Harris," amesema Freddy Ford.

Tangazo hili linakuja siku moja baada ya Bunge la Congress kuidhinisha matokeo ya uchaguzi wa rais wa mwezi Novemba, ambapo Joe Biden alimshinda rais wa sasa Donald Trump.

Hata hivyo rais anayemaliza muda wake Donald Trump anakataa kukubali kushindwa kwake katika uchaguzi huo na anatarajia kuzungumza leo Jumatano wakati wa maandamano huko Washington dhidi ya kuidhinishwa kwa matokeo ya uchaguzi.