MAREKANI

Maafisa wa polisi waliohusika katika kesi ya Jacob Blake kutoshtakiwa

Maandamano yaliyopita nchini Marekani kumtetea Jacob Blake
Maandamano yaliyopita nchini Marekani kumtetea Jacob Blake KAMIL KRZACZYNSKI / AFP

Maafisa wa polisi waliohusika katika kitendo cha kumpiga risasi na kumjeruhi vibaya Mmarekani mweusi Jacob Blake hawatashtakiwa, mwendesha mashtaka anayesimamia kesi hiyo ametangaza.

Matangazo ya kibiashara

Kitendo cha maafisa hao kilizusha maandamano makubwa nchini Marekani na katika nchi nyingi duniani na tayari wengi wamekosoa hatua hiyo na kusema kuwa inakuja  kuchochoea ghasia na inaonyesha kuwa ubaguzi wa rangi bado unaendelea nchini marekani.

"Kulingana na ukweli na sheria, tumeamua kwamba hakuna mashtaka yoyote yatakayozingatiwa" dhidi ya maafisa watatu waliohusika katika mkasa huo, mwendesha mashtaka wa eneo hilo Michael Graveley amesema katika mkutano na waandishi wa habari.

Michael Graveley amesema, afisa aliyafyatua risasi, Rusten Sheskey, alifanya vizuri katika hali ya kujihami.

Jacob Blake alikuwa anakabiliwa na mkono wa sheria baada ya kutolewa waranti wa kukamatwa dhidi yake kwa vurugu za nyumbani, amesema. Wakati maafisa wa polisi walipotaka kumkamata, "alijihami kwa kisu", amebaini Michael Graveley.

"Afisa wa polisi alifyatua risasi, baada ya kuona maisha yake yako hatarini."

Lakini hoja zake hazikushawishi wanasheria wa Jacob Blake. "Wanajaribu kufuta makosa yasiofutika," ameshutumu wakili wa familia B'Ivory Lamarr. "Ni aibu kubwa," ameongeza. Hii inaonyesha kuwa mnamo mwaka 2021, bado kuna mifumo mitatu ya haki: moja kwa weusi, moja kwa polisi na moja kwa Wamarekani wengine ”.