MAREKANI

Bunge la Seneti laidhinisha ushindi wa Joe Biden

Mike Pence makamu wa rais wa Marekani aliyesoma ushindi wa Biden katika bunge la Senate
Mike Pence makamu wa rais wa Marekani aliyesoma ushindi wa Biden katika bunge la Senate SAUL LOEB / AFP

Bunge la Seneti nchini Marekani limeidhinisha ushindi wa rais mteule Joe Biden, na kuruhusu mchakato wa kumkabidhi madaraka Januari 20. Joe Biden anakuwa rais wa 46 wa taifa hilo lenye nguvu duniani. 

Matangazo ya kibiashara

Kabla ya kufikia hatua hiyo, bunge lilijikuta limevamiwa na wafuasi wa rais anayemaliza muda wake Donald Trump na kusababisha vurugu katika majengo ya Capital Hill.

Watu wanee inadaiwa kuwa waliuawa katika makabiliano hayo kati ya vikosi vya usalama na wafuasi wa Donald Trump ambao walikuwa wanataka maseneta wabadili matokeo ya uchaguzi na kupinga ushindi wa Joe Biden, jambalo halikufanyika.

Hotuba ya Donald Trump ya kuwataka wafuasi wake kujielekeza mbele ya majengo ya Capitol Hill inasadikiwa kuwa ndio imechochea uvamizi huo.

Polisi katika eneo la Capitol walijibu maandamano hayo kwa kutumia bunduki na gesi ya kutoa machozi wakati mamia ya waandamanaji walipovamia na kutaka kulilaazimisha bunge kubatilisha ushindi wa Biden dhidi ya rais Donald Trump, muda mfupi baada ya Warepublican wenzake na Trump kuanzisha juhudi ya dakika za mwisho kutupilia mbali matokeo ushindi wa Biden.

Donald Trump aliwahimiza wafuasi wake waende Capitol wakati wa mchakato wa kuidhinisha ushindi wa Joe Biden. Mamia ya waandamanaji wanaomuunga mkono Trump waliandamana nje ya Bunge na kuingia ndani ya jengo hilo , na kusababisha kusitishwa kwa kikao na kuondolewa kwa maseneta ndani ya jengo hilo.

Polisi imechukua karibu saa nne kurejesha hali ya utulivu katika jengo hiulo baada ya kutumwa kwa vikosi vya walinzi wa kitaifa. Karibu saa 8 jioni kwa saa za Marekani, maseneta hatimaye waliweza kuanza tena kikao cha kuidhinisha ushindi wa Joe Biden.