MAREKANI

Joe Biden amteua Merrick Garland kuwa Waziri wa Sheria

Rais mteule wa Marekani, Joe Biden
Rais mteule wa Marekani, Joe Biden Angela Weiss / AFP

Rais mteule wa Marekani Joe Biden amethibitisha leo Alhamisi kuwa amemchagua Jaji Merrick Garland kuongoza wizara Sheria ya yenye ushawishi mkubwa nchini Marekani.

Matangazo ya kibiashara

Merrick Garland, mwenye umri wa miaka 68, kwa sasa ni mkuu wa Mahakama ya Rufaa ya Washington, chombo maarufu kwa umuhimu wa jinsi kinavyoshughulikia kesi mbalimbali zinazowakilishwa.

Joe Biden atamtambulisha waziri wake wa sheria na wajumbe wengine kadhaa, maafisa muhimu walioteuliwa kwenye wizara hiyo leo Ahamisi saa 7:30 saa za huko Wilmington, Delaware.

 "Uteuzi huu unaonyesha dhamira ya dhati ya rais mteule wa kuthibitisha (jukumu la) Idara ya Sheria kama nguzo ya uhuru na uadilifu, na kuhakikisha kuwa Waziri wa Sheria na timu yake ya karibu ni mawakili wa raia wa Marekani, na sio timu ya mawakili wa rais, ”taarifa ya timu ya Biden imesema.

 

Mapambano dhidi ya ubaguzi wa rangi

Merrick Garland atachukua nafasi ya Bill Barr, ambaye upinzani wa kutoka chama cha Democratic ulimpa jina la "Wakili wa Donald Trump" kwa sababu ya hatua zake nyingi kwa niaba ya rais anayemaliza muda wake au watu wake wa karibu.

Waziri wa baadaye, ikiwa uteuzi wake utathibitishwa na Bunge, atalazimika kubainisha uhuru wa wizara yake, kuwahakikishia baadhi ya wafanyikazi wake wapatao 110,000, lakini pia kuanzisha mageuzi makubwa yaliyoahidiwa na mgombea urais kutoka chama cha Democratic wakati wa kampeni yake.

Moja ya miradi ya kwanza ya Merrick Garland, itakuwa vita dhidi ya vurugu na ubaguzi wa rangi katika idara mbalimbali za polisi, mada iliyotawala kampeni baada ya kifo cha George Floyd, Mmarekani mweusi aliyefariki dunia akiwa mikononi mwa polisi mwishoni mwa mwezi Mei.

Uteuzi wa Merrick Garland unakuja siku moja baada ya kutaganzwa ushindi wa chama cha Democratic  katika uchaguzi muhimu wa maseneta katika jimbo la Georgia, na hivyo kudhibiti Baraza la Congress.