MAREKANI

Rais Donald Trump akubali kumalizika kwa muhula wake

Donald Trump, rais wa Marekani
Donald Trump, rais wa Marekani MANDEL NGAN AFP

Matukio ya machafuko huko Capitol Hill zitaendelea kuhusishwa na kumalizika kwa muhula wa rais wa Merika Trump, ambaye sasa anaonekana kutengwa katika kambi yake mwenyewe.

Matangazo ya kibiashara

Rais ameahidi mabadiliko ya mpangilio lakini bado hajakubali matokeo ya kura.

Baada ya mitandao ya kijamii Twitter, Facebook na YouTube kusimamisha kwa muda kurasa zake, rais Donald Trump amelazimika kutuma taarifa kwa vyombo vya habari akisema anakubali kuwa muhula wake umefikia ukingoni.

"Ingawa sikubaliani kabisa na matokeo ya uchaguzi, kutakuwa na kukabidhiana vizuri madaraka na mrithi wangu. Ingawa hii inaonyesa mwisho wa muhula mkuu wa kwanza katika historia ya rais nchi Marekani, ni mwanzo tu wa mapambano yetu kuifanya Marekani kuwa kubwa zaidi ”.

Hata hivyo hajalaani vurugu zilizotokea katika majengo ya Bunge la Seneti Capitol Hill na bado hatambui kushindwa kwake, ameripoti mwandishi wetu wa habari kutoka kitengo cha Kimataifa, Marie Normand.

Amekubali tu kumalizika kwa kipindi chake kama rais, hata kama anaonekana kutengwa kwenye uwanja wa kisiasa baada ya ghasia huko Washington.