MAREKANI

Rais Trump asema yuko tayari kukabidhi madaraka kwa amani

Rais wa Marekani Donald Trump
Rais wa Marekani Donald Trump (AP / JPP)

Rais wa Marekani Donald Trump anayeondoka madarakani ametoa mkanda wa video akilaani vurugu za wafuasi wake zilizoshuhudiwa katika eneo la Capitol Hill jijini Washington DC.

Matangazo ya kibiashara

Trump amesema kuwa kilicotokea hakikubaliki, yakiwa ni matamshi yake ya kwanza baada ya kufungiwa mitandao yake ya kijamii ya facebook na Twitter.

Aidha, Trump amesema kuwa kwa sasa nguvu zake anazipeleka kwenye kuhakikisha kuwa, kuna makabidhiano ya amani tarehe 20 mwezi Januari wakati rais mteule Joe Biden, atakapoapishwa.

“Kama wamerekanai wengine nimesikiishwa sana na vuruguvu zilizotokea, natuma maafisa wa usalama kudhibiti jengo la kuzuia vurugu zaidi, kwa sasa lengo langu ni kukabidhi madaraka kwa njia ya amani, "

"Huu ni wakati wa uponyaji na kuchukuliana, kwa wafuasi wangu najua mmesikitishwa sana lakini, fahamuni kuwa, safari yetu ndio inaanza,” amesema rais Trump.

Kauli hii ya Trump, imekuja baada ya bunge la Congress kuidhinisha ushindi wa Joe Biden na Makamu wake wa rais Kamala Harris.