MAREKANI

Trump kutohudhuria hafla ya kuapishwa Joe Biden

Donald Trump, rais wa Marekani
Donald Trump, rais wa Marekani Brendan Smialowski / AFP

Rais anaye maliza muda wake Donald Trump, ambaye alishindwa katika chaguzi wa urais wa mwezi Novemba, anaendelea kutengwa kisiasa, nchini humo.

Matangazo ya kibiashara

Trump ametangaza kwenye Twitter kwamba hatahudhuria hafla ya kuapishwa kwa Joe Biden mnamo Januari 20 huko Washington.

Huu ni moja ya jumbe za kwanza kupitia twitter za Donald Trump kutoa baada ya kupigwa mtandao waTwitter kuchukuwa hatua ya kusimamisha akaunti yake kwa saa 12.

"Kwa wale wote ambao wanapingana na suala hili, na sema sitahudhuria hafla ya kuapishwa Joe Biden Januari 20 ”.

Licha ya shinikizo kali la kisiasa tangu wafuasi wake kuvamia makao makuu ya Bunge la Seneti, Capitol Hill, siku ya Jumatano, licha ya kujiuzulu kwa maafisa kadhaa wa serikali yake, wakiwemo mawaziri wake wawili, Donald Trump anaendelea kupinga kushindwa kwake katika uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba.

Hata hivyo wengi kati ya wabunge kutoka chama cha Democratic wanahoji afya ya akili ya rais Donald Trump, na wamependekeza bunge kuchukuwa hatua ili kumtimuwa rais Trump kweye wadhifa wake, ambapo anasalia na siku 12 katika uongozi wa nchi.