MAREKANI

Twitter yasitisha kabisa akaunti ya kibinafsi ya Donald Trump

Donald Trump, rais wa Marekani
Donald Trump, rais wa Marekani MANDEL NGAN / AFP

Rais wa Marekani anaye maliza muda wake Donald Trump hawezi tena kutumia ukurasa wake wa twitter kwa mawasiliano yoyote baada ya mtandao huo kuamua kusitisha moja kwa moja akaunti yake.

Matangazo ya kibiashara

Idara ya huduma ya microblogging ya mtandao wa kijamii wa Twitter  imeamua kusitisha 'moja kwa moja' akaunti ya rais wa Marekani ili kuepusha "wito zaidi wa vurugu".

Katika barua ya blogi, Twitter imebainisha "kuwa wametathmini jumbe za hivi karibuni za Donald Trump kwa uangalifu" na kubaini kwamba ni hatari kwa usalama wa nchi.

Akaunti ya rais wa Marekani, aliyeshindwa katika uchaguzi wa urais wa mwezi Novemba, ilikuwa tayari imesimamishwa kwa saa 12 baada ya wafuasi wake kufanya uvamizi katika makao makuu ya Bunge la Seneti, Capitol Hill.

Kwa hivyo Donald Trump anapoteza mawasiliano na watu milioni 89 waliokuwa wakimfuata kupitia mtandao aw Twitter.