BRAZIL-COVID 19

Ugonjwa wa Covid-19 washika kasi Amerika ya Kusini

Baada ya miezi mitatu ya kupungua kwa visa vya maambukizi, tangu kiwango cha juu kama hicho kufikiwa mwishoni mwa mwezi Julai, idadi ya kila siku ya maambukizi imeongezeka tena nchini Brazil.
Baada ya miezi mitatu ya kupungua kwa visa vya maambukizi, tangu kiwango cha juu kama hicho kufikiwa mwishoni mwa mwezi Julai, idadi ya kila siku ya maambukizi imeongezeka tena nchini Brazil. REUTERS

Brazil ni nchi ya pili iliyoathirika zaidi duniani na virusi vya Corona, baada ya Marekani. Nchi hii imevuka kizingiti cha vifo vya watu 200,000.

Matangazo ya kibiashara

Janga hilo pia linaripotiwa kuongezeka nchini Mexico na Argentina. Kutokana na hali hii, serikali nyingi zimeongeza hatua za kuzuia kuenea kwa virusi vya Corona.

Muda wa hali ya dharura ya kiafya umerefushwa katika mji mkuu wa Mexico, kulinagana na meya wa mji huo, baada ya mji huo tangu wiki mbili zilizopita kushuhudia ongezeko la visa vya maambukizi lisilo la kawaida.

Hospitali nyingi zimejaa wagonjwa, huku vitanda karibu 90% vimelazwa wagonjwa mahututi wa COVID-19. Kwa hivyo hakuna swali la kuondoa vizuizi. Shughuli muhimu tu zimeruhusiwa, kama uchukuzi shughuli za benki.

Kwa upande wake, Argentina imeongza hatua kudhibiti kunea kwa virusi vya Corona. Sheria ya kutotoka nje usiku na marufuku ya watu kutembea imetangazwa katika mikoa saba kati ya 23 nchini humo.

Kulingana na mamlaka, ongezeko la maambukizi limesababishwa na sikukuu za mwisho wa mwaka, lakini pia na mikusanyiko mikubwa. Mwishoni mwa mwezi wa Novemba, makumi ya maelfu ya Waargentina walikusanyika Buenos Aires kwa mazishi ya mwanasoka maarufu Diego Maradona.

Argentina bado imeanza kampeni yake ya chanjo, tofauti na jirani yake Brazil.

Brazil, ambayo inaweza hivi karibuni kuidhinisha chanjo dhidi ya COVID-19 kutoka kampuni ya China Sinovac. Katika nchi hii, idadi ya vifo kutokana na Covid-19 iliongezeka kwa 65% mwezi uliopita.