MAREKANI

Utoaji wa chanjo dhidi ya COVID-19 wazua mkanganyiko na utata Texas

Chanjo iliyotengezwa na kampuni ya  Pfizer na BioNTech.
Chanjo iliyotengezwa na kampuni ya Pfizer na BioNTech. REUTERS/Brendan McDermid/File Photo

Wakati jimbo la Texas likirekodi vifo 28,545 kutokana na virusi vya Corona , hospitali nyingi zimejaa wagonjwa na baadhi zinakabiliwa na ukosefu wa vitanda vya kulaza wagonjwa mahututi.

Matangazo ya kibiashara

Wengi walitarajiwa zoezi la utoaji chanjo, lakini tangu kuanza kwa kampeni hii 0.17% pekee ndi tayari wamepewa chanjo hiyo.

Serikali imeachia mamalaka ya kila jimbo kujishughulisha na zoezi la utowaji chanjo kwa wakaazi wake, lakini katika jimbo laTexas zoezi hilo limezua mkanganyiko na utata.

Tangu katikati ya mwezi Desemba, dozi milioni 1.4 zimepelekwa katika jimbo la Texas, lakini ni wakaazi 475,000 tu ndio wamepokea chanjo ya kwanza kwa njia ya kudungwa sindano, na watu 6,500 wamepata chanjo mbili. Na karibu hospitali 30 za vijijini hazijapokea dozi yoyote ya chanjo ya COVID-19, licha ya kuthibitishwa kama vituo vya chanjo.

Kwa jumla, kati ya wakaazi milioni 30 wa Texas, milioni 8 wako katika kundi la watu kupewa chanjo ya haraka: wazee wenye umri wa zaidi ya miaka 65, wafanyikazi wa hospitali.