MAREKANI

Wabunge kutoka chama cha Democratic waapa kumng'oa Donald Trump mdarakani

Spika wa bunge la wawakilishi  Nancy Pelosi
Spika wa bunge la wawakilishi Nancy Pelosi REUTERS/Jonathan Ernst

Wabunge wa chama cha Democratic wakiungwa mkono na baadhi ya wabunge kutoka chama cha Republican wanatarajia kuanza utaratibu wa kumtimuwa Donald Trump kwenye wadhifa wake, wakibaini kwamba ameshindwa kutekeleza majukumu yake vilivyo

Matangazo ya kibiashara

Wabunge wa Democrats wanapanga kumshtaki bungeni rais Trump kwa 'malipo ya uasi' dhidi ya hatua yake ya 'kuchochochea ghasia' zilizosababisha uvamizi wa jumba la Bunge la Capitol Hill.

Hata hivyo wabunge kutoka chama cha Democratic wanapanga kwanza kumuomba Makamu wa Rais Mike Pence kumtaka mwenyewe rais wake aachie ngazi.

Siku nne baada ya tukio la kuhuzunisha katika makao makuu ya Bunge la seneti Capitol Hill, lililosababisha vifo vya watu watano.

Spika wa Bunge Nancy Pelosi alitangaza mfululizo wa hatua za kumwondoa mamlakani rais kutoka chama cha Republican, aliyetajwa kama "tishio " dhidi ya demokrasia na Katiba ya Marekani.

Hatua ya kwanza: kutoa wito kwa kwa Mike Pence kuchukuwa hatua ya kumtaka rais wake aachie ngazi.

Siku ya Jumapili Wabunge walionya kwamba wako tayari kuanzisha utaratibu mpya wa kihistoria wa kumng'atua madarakani Donald Trump katika siku zijazo.