MAREKANI

FBI yasema maandamano zaidi yamepangwa nchini Marekani

Maandamano yaliyopita, ya kumuunga mkono rais Donald Trump
Maandamano yaliyopita, ya kumuunga mkono rais Donald Trump ANDREW CABALLERO-REYNOLDS / AFP

Idara ya upelelezi nchini Marekani nchini Marekani FBI inaonya kuwa huenda kukashuhudidwa maandamano ye nye ghasia nchini Marekani kuelekea kuapishwa kwa rais mteule Joe Biden.

Matangazo ya kibiashara

FBI inasema katika ripoti yake kuwa, kuna makundi yenye silaha yanayopanga maandamano hayo yenye fujo katika majimbo yote 50 nchini humo kuelekea kuapishwa kwa Joe Biden na Makamu wa rais mteule Kamala Harris tarehe 20 mwezi Januari.

Ripoti hii ya FBI inazua wasiwasi wa usalama kuelekea kuapishwa kwa Biden katika eneo la Capitol Hill.

Biden amesema haogopi kuapishwa katika eneo hilo ambao lilishuhuhudia vurugu wiki iliyopita, baada ya wafuasi wa rais anayeondoka madarakani Donald Trump kuvamia majengo ya bunge la Congress na lile la wawakilishi kujaribu kuzuia kuidhinishwa kwa ushindi wa Biden.

Wakati hayo yakijiri, Trump ametangaza hali ya hatari katika jiji kuu Washington na kuamuru usalama kuimarishwa wakati huu Kaimu Waziri wa usalama wa ndani Chad Wolf akijiuzulu, na kufikisha idadi ya mawaziri waliojizulu katika serikali ya Trump tangu kuzuka kwa fujo hizo kufikia watatu.