MAREKANI

Pence akataa mchakato wa kumwondoa Trump madarakani

Rais wa Marekani anayeondoka madarakani Donald Trump
Rais wa Marekani anayeondoka madarakani Donald Trump REUTERS/Leah Millis

Wabunge wa bunge la Wawakilishi nchini Marekani wanajadili mswada wa kumtaka Makamu wa rais Mike Pënce kutumia kifungu cha katiba namba 25 kumwondoa rais Donald Trump madarakani kufuatia wafausi wake kuandamana na kuzua fujo katika majengo ya bunge wiki iliyopita katika eneo la Capitol Hill.

Matangazo ya kibiashara

Hata hivyo, Pence kwa barua yake kwa wabunge hao amesema hatua hiyo ya busara kwa sasa na sio kwa maslahi mapana kwa taifa hilo.

Naye Trump anayeondoka madarakani amesema hatua hiyo ya bunge ni hatari kwa Marekani.

“Matumizi ya kifungu nambari 25 hakina athari kwangu, nitakuja kumtesa Joe Biden na uongozi wake, kama wanavyosela kuwa makini kile unachokitaka,

kinachoendelea ni mwendelzo wa kuniwinda hali ambayo inaendelea kusababisha hasira , mgawanyiko na chuki, na huenda lisieleweke sasa hivi lakini, ni hatari kwa Marekani hasa katika kipind hiki,” alisema.

Mmoja wa viongozi wa chama cha Republican char ais Trump, Liz Cheney amesema atapiga kura ya kumwondoa madarakani rais huyo kufuatia vurugu za wiki iliyopita.

Rais wa Marekani anayeondoka madarakani ifikapo tarehe 20 Januari Donald Trump hajawahi kukubali kushindwa kwenye Uchaguzi wa Novemba mwaka 2020, uliompa ushindi Joe Biden.