MAREKANI

Zaidi ya watu milioni 10 wapewa chanjo Marekani

Chanjo ya Pfizer
Chanjo ya Pfizer REUTERS/Dado Ruvic/Illustration/File Photo

Zaidi ya Wamarekani milioni 10 wamepata dozi ya kwanza ya chanjo dhidi ya Corona, kulingana na takwimu kutoka Vituo vya Udhibiti na Kuzuia Magonjwa vya Marekani (CDC).

Matangazo ya kibiashara

Kizingiti cha dozi milioni 10 zilizotolewa kilivuka siku moja baada ya utawala wa Trump kutangaza agizo jipya linaloyataka majimbo ya Marekani kuwapa chanjo watu wote wenye umri wa miaka 65 na zaidi, na sio tu wahudumu wa afya.

Kulingana na hesabu ya shirika la habari la REUTERS, siku ya Jumanne Marekani ilirekodi rekodi ya vifo vya kila siku vilivyotokana na janga hilo, sawa na vifo vipya 4,336.

Idadi ya vifo nchini Marekani ni zaidi ya 380,000 wakati zaidi ya visa milioni 22 vya maambukizi vimeripotiwa.

Karibu dozi milioni 30 za chanjo zinazotengenezwa na maabara ya Moderna na Pfizer hadi sasa zimesambazwa nchini.