MAREKANI

Joe Biden kuapishwa rais wa Marekani Jumatano, maandalizi yakamilika

Rais mteule wa Marekani Joe Biden
Rais mteule wa Marekani Joe Biden Angela Weiss / AFP

Rais mteule wa Marekani Joe Biden, anatarajiwa kuapishwa siku ya Jumatano katika jiji kuu la Washington DC baada ya kumshinda rais Donald Trump, wakati wa Uchaguzi Mkuu mwezi Novemba mwaka 2020.

Matangazo ya kibiashara

Kinyume na miaka iliyopita, kuna idadi kubwa ya wanajeshi jijini Washington DC baada ya taarifa kuwa huenda kukatokea na maandamano ya fujo ya wafuasi wa Trump katika jiji hilo.

Tahadhari hii imechukuliwa baada ya wafuasi wa Trump wiki mbili zilizopita, kuvamia majengo ya bunge la wawakilishi na Senate wakati mjadala wa kuidhinisha ushindi wa Biden ulipokuwa unaendelea.

Rais Trump ambaye anaondoka madarakani, amekataa mara kadhaa kutambua ushindi wa Biden na tayari amesema kuwa hatakuwepo kwenye sherehe za kumwapisha Biden.

Miongoni mwa maamuzi ya kwanza ambayo Biden anatarajiwa kuchukua baada ya kuingia madarakani, ni kurejesha kuzuizi cha watu kuingia nchini humo, kutoka katika mataifa ambayo yanshuhudia maambukisi makubwa hasa barani Ulaya na huko Brazil.

Biden anaingia madarakani katika kipindi ambacho nchi yake inakabiliwa na janga la Corona, na kushinda virusi hivyo ndio itakuwa kazi yake ya kwanza atakapoindia madarakani.

Idadi ndogo tu ya watu ndio itakayoruhusiwa kushuhudia sherehe hizo za kumwapisha Biden kuwa rais wa 46 wa Marekani.