MAREKANI

Rais Biden aanza kazi baada ya kuapishwa

Rais mpya wa Marekani Joe Biden akiapa Januari 20 2021
Rais mpya wa Marekani Joe Biden akiapa Januari 20 2021 REUTERS/Kevin Lamarque

Rais mpya wa Marekani Joe Biden, ameanza kazi baada ya kuapishwa yeye pamoja na Makamu wake,Kamala Harris mwanamke wa kwanza katika nafasi hiyo ya juu katika historia ya siasa za Marekani. 

Matangazo ya kibiashara

Rais Biden mwenye umri wa mika 78 , amekuwa rais wa 46 wa Marekani na baada ya kuapa, kupitia ukurasa Wake wa Twitter, amesema hakuna muda wa kupoteza na sasa kazi inaanza kutatua changamoti zinazolikabili taifa hilo, na amesaini maagizo kadhaa kubadilisha maamuzi yaliyofanywa na mtangulizi wake Donald Trump.

Katika hotuba yake ya kwanza, muda mfupi baada ya kuapishwa, Biden alisema, demokrasia imeshinda.

“Maamuzi ya watu yamesikika , na kuheshimika, tumejifunza kuwa demokrasia ni kitu cha thamani  sana na sio cha kuchezea, katika muda huu rafiki zangu, demokrasia imeshinda,” alisema rais Biden.

Miongoni mwa mambo makubwa ambayto rais Biden ametoa maagizo mapya ni pamoja na mbinu mpya za kukabiliana na janga la Corona, na sasa ni lazima kuvcalia barakoa katika maeneo yote ya umma na majengo ya serikali.

Aidha, ametia saini michakato ya Marekani kurejea tena kama mwanachama wa Shirika la afya duniani WHO lakini pia kwenye mkataba wa kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi, mkataba ambao uogozi uliopita wa Trump ulikuwa umejiondoa.

Rais Biden pîa ameagiza kusitishwa kwa mpango wa serikali iliyopita, kujenga ukuta kati ya Marekani na Mexico, lakini pia ameondoa marufuku ya watu kutoka baadhi ya mataifa ya Kiislamu kuja Marekani.

Kiongozi wa kwanza wa nje anayetarajiwa kuzugumza na rais mpya wa Marekani siku ya Ijumaa, ni Waziri Mkuu wa Canada Justin Trudeau.