CHINA-MAREKANI

Siku ya kuapishwa kwa Joe Biden, China yawawekea vikwazo maofisa wa Trump

Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo
Aliyekuwa waziri wa mambo ya nje wa Marekani, Mike Pompeo Mike Segar/Reuters

China, hasimu wa kimfumo wa Marekani katika kinyang'anyiro cha nafasi ya nchi yenye nguvu duniani, imetangaza vikwazo dhidi ya utawala wa Donald Trump, saa chache baada ya kuapishwa rais mpya Joe Biden.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni hatua ya kwanza ya China saa chache baada ya kuapishwa Joe Biden kama rais wa Marekani.

China imetaka kuonya utawala mpya kwa kuuwekea vikwazo utawala unaoondoka.

Beijing imekuwa ikisubiri kuondoka kwa Donald Trump ili kutoa taarifa yake. Saa moja asubuhi kwa saa za China: majina 28 ya maafisa wa Marekani yamenekana kwenye tovuti ya Wizara ya Mambo ya nje ya China.

Washauri wa Ikulu ya White House Peter Navarro, Robert O'Brien na Matthew Pottinger, Naibu waziri wa mambo ya nje katika ukanda wa Asia ya Mashariki David Stilwell, Katibu wa Afya Alex Azar, Mwakilishi wa Marekani kwenye Umoja wa Mataifa Kelly Craft, lakini pia washauri wa zamani wa Donald Trump, John Bolton na Stephen Bannon, bila kusahau Mike Pompeo, waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani ni miongoni mwa maafisa wa utawala wa zamani wa Donald Trump ambao wamewekewa vikwazo na China. Wote, pamoja na familia zao, sasa wamepigwa marufuku kuingia Jamhuri ya Watu wa China na vile vile mikoa maalum ya utawala ya Hong Kong na Macao.

 

Kauli yenye sauti ya uchungu: Beijing haisahau kwamba baadhi ya "wanasiasa wanaopinga China, kwa sababu ya masilahi yao ya kisiasa ya ubinafsi, chuki yao dhidi ya China […] walipanga, kuendeleza na kutekeleza vitendo viovu na kuingilia sana mambo ya ndani ya China, huku wakidhoofisha masilahi ya China, waliwaudhi raia wa China na kuvuruga uhusiano [kati ya nchi hizo mbili]. "

 

"Kuweka vikwazo hivi siku ya kuapishwa kwa raias mpya inaonekana kuwa ni jaribio la kunyemelea kwenye mgawanyiko unaoendelea," Emily Horne, msemaji wa Baraza la Usalama la Kitaifa katika Ikulu White House, ameliambia shirika la Habari la Reuters katika taarifa. Wamarekani kutoka pande zote mbili wanapaswa kulaani hatua hii isiyo na tija na ya kijinga. Rais Biden anatarajia kufanya kazi na viongozi wa pande zote mbili kuiweka Marekani kuchukua nafasi ya China. "

 

Antony Blinken, mwanadiplomasia mwenye uzoefu aliyechaguliwa na Joe Biden kwa wadhifa wa Waziri wa mambo ya Nje, alisema katika kikao cha uthibitisho mbele ya kamati ya Seneti Jumanne kwamba China "bila shaka" inawakilisha changamoto muhimu zaidi kwa Marekani na nchi nyingine yoyote.

 

Ishara ya kwanza ya rais mpya wa Marekani kuunga mkono Taiwan, mwakilishi wa Taiwan nchini Marekani alialikwa rasmi kwenye sherehe ya kuapishwa kwake.