MAREKANI

Kesi ya mashtaka ya Trump kuanza Februari 8 katika Bunge la Seneti

Rais wa zamani wa Marekani  Donald Trump
Rais wa zamani wa Marekani Donald Trump Brendan Smialowski / AFP

Kesi ya rais wa zamani wa Marekani itaanza wiki ya pili ya Februari katika Bunge la Seneti, baada ya kuwasilishwa mashitaka katika taasisi hiyo mapema wiki ijayo, maafisa wa chama cha Democratic katika Baraza la Congress wamesema.

Matangazo ya kibiashara

"Mara baada ya faili hizo kutayarishwa, kesi itaanza wiki ya Februari 8," amesema Chuck Schumer, kiongozi wa chama cha Democratic katika Bunge la Seneti, ambapo Donald Trump atasikilizwa kwa madai ya "kuchochea uasi".

Chuck Schumer hapo awali alikuwa amewaambia wenzake kwamba mashtaka "yatapelekwa katika Bunge la Seneti Jumatatu".

Kucheleweshwa kwa wiki mbili kati ya kuwasilishwa kwa mashtaka na kuanza kwa mjadala hakutampa tu rais wa zamani Donald Trump muda zaidi wa kuandaa utetezi wake.

Pia kutawezesha kesi hiyo kutochukuwa muda mrefu ii kukataa kuzorotesha shughuli za taasisi hiyo wakati muhula wa Joe Biden unaanza. Wakati huo Bunge la Seneti litakua likijianda katika shughuli ya kuidhinisha wajumbe wa wa serikali ya Joe Biden.

Chuck Schumer amesema asubuhi kuwa amejadiliana na kiongozi wa wengi wa chama cha Republican Mitch McConnell kuhusu "ratiba na muda" wa vikao.

Mitch McConnell alikuwa amependekeza kusubiri hadi katikati ya mwezi Februari ili kuanza kwa mijadala. "Mashtaka ya Bunge yamekuwa ya haraka na ya chini zaidi kuliko hapo awali, hatua inayofuata haiweziitatuchukuwa muda," amesema.

Tunahitaji kesi iliyo wasi na ya kweli, ambapo rais wa zamani anaweza kujitetea na Bunge la Seneti kuweza kuzingatia maswala yote ya ukweli, ya kisheria na ya kikatiba. "

Kufikia sasa, Joe Biden amejizuia kuingilia kati suala hili, akibaini kwamba ni kwa Bunge la Seneti lenyewe kuweka masharti ya kesi ya mtangulizi wake.

Donald Trump anatuhumiwa kuwa aliwahimiza wafuasi wake kuanzisha shambulio katika majengo ya Bunge la Seneti, Capitol Hill,  Januari 6, wakati wawakilishi wabunge na maseneti walikuwa wakiidhinisha ushindi wa Joe Biden aliyetangazwa kushinda uchaguzi wa urais.