MAREKANI-CHINA

Marekani na China uso kwa uso katika Bahari ya China

Mpaka wenye mzozo katika eneo la Sikkim
Mpaka wenye mzozo katika eneo la Sikkim Agnes BUN / AFP

Mvutano unaendelea kati ya Marekani na China katika bahari ya Kusini mwa China huku  meli za kivita zikiegeshwa  katika bahari hiyo tangu Jumapili.

Matangazo ya kibiashara

Marekani inasema inapiga kambi katika bahari hiyo kwa ajili ya kutetea "uhuru wa kusafiri katika maji ya kimataifa".

Lakini hii inaashiria Beijing kwamba Washington iko tayari kutetea Taiwan dhidi ya uvamizi wowote.

Meli nne kubwa za kivita ziliwasili katika Bahari ya Kusini mwa China Jumapili, siku ambayo Taiwan ilitangaza kwamba iliona juu ya anga yake ndege thelathini za kivita kutoka China mwishoni mwa wiki hii iliyopita.

Kama mazoezi ya kijeshi yamekuwa ya kawaida katika miezi ya hivi karibuni, kwa sasa yamefikia hatua mpya. Kwa sababu vifaa vilivyotumwa ni vya aina ya mashambulizi, na sio kujihami kama ilivyokuwa awali, na kuilazimu Taiwan kupeleka mfumo wake wa kupambana dhidi ya makombora.

China haijatoa maelezo juu ya mazoezi hayo makubwa ya kijeshi, lakini inaonekana hawakupendelea ishara za kwanza za utawala wa Biden kwa Taiwan. Hasa, mwaliko wa mwakilishi wa Taiwan kwenye sherehe ya kuapishwa kwa Joe Biden Jumatano wiki iliyopita.

Msemaji wa wizara ya mambo ya nje ya Marekani ilisema wakati huo kwamba "Beijing lazima imalize shinikizo lake la kijeshi, kidiplomasia na kiuchumi kwa Taiwan, na kushiriki mazungumzo ya kujenga na mamlaka ya Taiwan. "