MEXICO

Idadi ya vifo yapindukia zaidi ya 150,000 Mexico

Afisa wa afya nchini Mexico
Afisa wa afya nchini Mexico REUTERS/Edgard Garrido

Mexico imerekodi visa vipya 8,521 vya maambukizi ya virusi vya Corona na vifo 659 vilivyotokana na janga hilo katika muda wa saa ishirini na nne zilizopita, Wizara ya Afya imeripoti, siku moja baada rais Andres Manuel Lopez Obrador kupatikana na maambukizi ya Corona.

Matangazo ya kibiashara

Andres Manuel Lopez Obrador havai barakoa katika maeneo ya umma. Alionekana tu akivaa barakoa wakati aliposafiri kwa ndege.

Rais wa Mexico Andres Manuel Lopez anafahamika kwa kupuuza kitisho cha janga la virusi vya Corona.

Bwana Lopez Obrador, ambaye aliagiza raia wake kuendelea kufanya shughuli zao mbalimbali wakati wa janga hilo, jana Jumatatu alimteua Katibu wa Mambo ya Ndani Olga Sánchez kuchukua nafasi yake katika mkutano wake na waandishi wa habari Jumatatu hadi Ijumaa saa moja asubuhi kwa saa za Mexico.

Kulingana na takwimu za serikali, idadi ya visa vya maambukizi sasa imefikia 1,771,740 na vifo 150,273.