MAREKANI

Mashtaka dhidi ya Trump yawasilishwa rasmi mbele ya Bunge la Seneti

Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani
Donald Trump, rais wa zamani wa Marekani REUTERS/Carlos Barria

Maseneta wa Marekani wameapishwa leo Jumanne subuhi kuwa mawakili katika kesi ya Donald Trump.

Matangazo ya kibiashara

Hii ni mara ya kwanza katika historia ya Marekani rais kukabiliwa na mchakato huu wa mashtaka mara mbili.

Waendesha mashtaka kutoka Baraza la Wawakilishi waliwasilisha, Jumatatu jioni, mashtaka mbele yaBunge la Seneti, na kwa hivyo kutoa nafasi ya kuanza rasmi kwa kesi hiyo.

Ni tukio adhimu sana ambalo limetokea mara nne tu katika historia ya Marekani. Wabunge kutoka baraza la Wawakilishi, ambao watakuwa waendesha mashtaka wakati wa kesi hiyo, walivuliwa wadhifa huo kwa muda na kwenda kuketi katika Bunge la Seneti.

Timu hii ya waendesha mashitaka tisa kutoka Baraza la Wawakilishi itaongozwa na Jamie Raskin ambaye alisoma hivi karibuni mashitaka dhidi ya Donald Trump.

Donald Trump anashtumiwa kuchochea ghasia. Hotuba yake aliyoitoa kabla ya uvamizi huo imetajwa katika barua hiyo ya mashitaka.

Wafuasi wa Trump walivamia majengo ya Bunge la Seneti, Capitol Hill ili kupinga kuidhinishwa ushindi wa Joe Biden, aliyeshida katika uchaguzi wa urais uliyofanyika mwezi Novemba 2020.

Kesi yenyewe imepangwa kuanza Februari 9. Muda huu ulijadiliwa kumruhusu Donald Trump kuandaa utetezi wake.