Ecuador: Zaidi ya 62 wafariki dunia baada ya makabiliano katika jela
Imechapishwa:
Watu wasiopungua 62 wamepoteza maisha katika makabiliano katika magereza kadhaa nchini Ecuador siku ya Jumanne.
Rais wa Ecuador Lenin Moreno ametangaza hali ya dharura ya muda ya mamlaka ya magereza katika jaribio la kurejesha utulivu katika magereza ya nchi hiyo, ambapo ghasia zinazosababishwa na makundi hasimu hutokea mara kwa mara.
"Makundi mawili yalikuwa yanatafuta udhibiti wa magereza," amesema Edmundo Moncayo, mkurugenzi wa mamlaka ya magereza nchini Ecuador.
Amebaini kwamba polisi 800 wa ziada wametumwa katika magereza mbalimbali na kwamba "hali ya utukivu imerejeshwa katika magereza."
Makabiliano hayo yalizuka katika magereza ya Guayas, Azuay na Cotopaxi, ambayo yana karibu 70% ya wafungwa, kulingana na takwimu rasmi.