MAREKANI-AFYA

Chanjo ya Johnson & Johnson kuthibtishwa kuwa salama Marekani

Uwezo wa chanjo ya Johnson & Johnson, umethibitishwa baada ya kufanyiwa kwa majaribio ya chanjo hiyo nchini Afrika Kusini, Brazil na Marekani,
Uwezo wa chanjo ya Johnson & Johnson, umethibitishwa baada ya kufanyiwa kwa majaribio ya chanjo hiyo nchini Afrika Kusini, Brazil na Marekani, Michael Ciaglo GETTY IMAGES NORTH AMERICA/AFP/File

Watalaam wa kudhibiti matumizi ya chanjo nchini Marekani, sasa wanasema kuwa chanjo ya kudhibiti maambukizi ya Corona  iliyotenengezwa na kampuni ya Johnson & Johnson, inafanya kazi kwa kiwango kikubwa kwa mtu kupewa dozi moja tu na ni salama.

Matangazo ya kibiashara

Chanjo ya Johnson & Johnson, inatarajiwa kuwa ya tatu kuthibtishwa na maafisa wa Marekani kuwa salama na kuanza kutumiwa kushinda maambukizi ya Corona.

Imebainika kuwa, tofauti na chanjo za Pfizer na Moderna, chanjo hii haina ulazima wa kuhifadhiwa kwenye baridi kali.

Uwezo wa chanjo hii, umethibitishwa baada ya kufanyiwa kwa majaribio ya chanjo hiyo nchini Afrika Kusini, Brazil na Marekani, nchi ambazo zimekuwa zimeendelea kushuhudia maambukizi makubwa duniani.

Usalama wa chanjo hiyo, umebainika pia baada ya kutotokea kwa kifo chochote kati ya watu wote waliopewa chanjo hiyo kwa majaribio na hakuna aliyelazwa hospitalini kwa kupokea chanjo hiyo.