Makabiliano katika jela Ecuador: Idadi ya vifo yaongezeka hadi 79
Imechapishwa: Imehaririwa:
Serikali ya Ecuador imetangaza kuwa idadi ya vifo katika magereza kadhaa nchini humo imeongezeka hadi 79 na watu kadhaa wamejeruhiwa katika makabiliano kati ya makundi hasimu.
Ingawa maafisa wanadai kuwa wamerejesha utulivu katika magereza ambapo ghasia zilitokea, mkuu wa polisi wa kitaifa ametangaza kwamba makabioliano kati ya makundi hasimu yalikuwa yakiendelea Jumatano jioni katika gereza la Guayaquil.
Maafisa wa polisi na wanajeshi wamepelekwa katika magereza huko Guayaquil, Cuenca na Latacunga ambapo makundi hasimu yalikabiliana siku ya Jumanne.
Mamlaka ya magereza nchini Ecuador (SNAI) imeisema wafungwa 75 walipoteza wakati wa ghasia hizo. Kulingana na takwimu rasmi, wafungwa kadhaa na polisi walijeruhiwa.
SNAI imethibitisha kuwa makabiliano yalikuwa yakiendelea Jumatano, ikitaja kwamba maafisa wake na polisi walikuwa wakiratibu operesheni yao bila kutoa maelezo zaidi.