MAREKANI-AFYA-UCHUMI

Coronavirus: Jopo la wataalam lapendekeza idhini ya chanjo ya J & J Marekani

Wataalam wanasema chanjo ya Johnson & Johnson dhidi ya COVID-19 itakuwa nyenzo nyingine muhimu katika kumaliza janga hilo Marekani, ambapo zaidi ya watu 500,000 wamefariki dunia.
Wataalam wanasema chanjo ya Johnson & Johnson dhidi ya COVID-19 itakuwa nyenzo nyingine muhimu katika kumaliza janga hilo Marekani, ambapo zaidi ya watu 500,000 wamefariki dunia. Mark RALSTON AFP/File

Jopo la wataalam huru linashauri mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA) kupigia kura kwa kauli umoja kuidhinishwa kwa chanjo ya COVID-19 kutoka kwa maabara ya Johnson & Johnson (J&J) siku ya Ijumaa.

Matangazo ya kibiashara

Sasa ni kwa mamlaka ya FDA kutoa idhini yake ya matumizi ya dharura ya chanjo ya tatu nchini Marekani, ya kwanza kwa dozi ya kutumia mara moja, hali ambayo inaweza kufanyika katika siku zijazo.

Mamlaka ya Chakula na Dawa nchini Marekani (FDA) ilikuwa imefuata mapendekezo ya wataalam wa chanjo mbili ya Pfizer-BioNTech na ile ya Moderna.

Maabara ya J & J imesema iko tayari kutoa kati ya dozi milioni tatu hadi nne kuanzia wiki ijayo ikiwa chanjo yake itaidhinishwa.