MAREKANI-SIASA-UCHUMI

Biden atengua uteuzi wa Tanden kuongoza ofisi ya bajeti

Rais wa Marekani Joe Biden  akubali kutengua uteuzi wa Neera Tanden kuongoza Ofisi ya Urasibu na Bajeti ya Ikulu White House kufuatia upinzani kutoka baadhi ya wabunge wa chama chake cha Democratic.
Rais wa Marekani Joe Biden akubali kutengua uteuzi wa Neera Tanden kuongoza Ofisi ya Urasibu na Bajeti ya Ikulu White House kufuatia upinzani kutoka baadhi ya wabunge wa chama chake cha Democratic. REUTERS - JONATHAN ERNST

Rais wa Marekani Joe Biden amesema ametengua uteuzi wa Neera Tanden kuongoza Ofisi ya Urasibu na Bajeti ya Ikulu White House (OMB), kikwazo chake cha kwanza katika kuunda utawala wake.

Matangazo ya kibiashara

Hatua hiyo inakuja wakati uteuzi wa Neera Tanden kuongoza ofisi hiyo ulisababisha upinzani mkali kati ya wabunge na maseneta nchini humo.

Tangazo hilo limekuja wakati Bunge la Seneti hapo jana Jumanne lilipiga kura kudhibitisha wagombea kadhaa waliochaguliwa na Joe Biden kwenye nyadhifa mbalimbali katika utawala wa shirikisho.

Maseneta wengi wamethibitisha uteuzi wa Cecilia Rouse kama rais wa Baraza la Uchambuzi wa Kiuchumi katika Ikulu ya White House, baada ya kuthibitisha uteuzi wa Gina Raimondo kama Katibu wa Biashara.

"Nimekubali ombi la Neera Tanden kuondoa jina lake kwenye uteuzi wa mkurugenzi wa Ofisi ya Urasibu na Bajeti," Joe Biden alisema katika taarifa fupi.

Uamuzi huu unaonyesha udhaifu wa udhibiti ambao Wademocrats wanao katika Bunge la Seneti, ambalo llinapaswa kuidhinisha wagombea waliochaguliwa na rais wa Marekani kwa nafasi kadhaa muhimu katika utawala wa shirikisho.

Ikiwa Wademocrats na Warepublican wana idadi sawa (50) ya viti katika Bunge la Seneti, Makamu wa rais Kamala Harris anaweza kuingilia kati ikiwa kuna usawa wakati wa kupiga kura ili kupigia kura kwa niaba ya Wademocrats.

Lakini uteuzi huo haukuwezekana tena baada ya Seneta wa kutoka chama cha Democratic Joe Manchin, mwenye msimamo wa wastani, kuonyesha kwamba atapigia kura dhidi ya uthibitisho wa Neera Tanden, mkurugenzi wa sasa wa Kituo cha think-tank Center for American Progress

Ikulu ya White House- na Neera Tanden - wamejaribu kupata uungwaji mkono wa maseneta kutoka chama cha Republican, bila mafanikio, licha ya mkutano wa dakika ya mwisho Jumatatu na Seneta kutoka chama cha Republican Lisa Murkowski.