BRAZILI-AFYA

Coronavirus: Bolsonaro awataka Wabrazili kuacha kunung'unika

Rais Bolsonoro katika mkutano na waandishi wa habari huko Brasilia, Machi 5, 2021.
Rais Bolsonoro katika mkutano na waandishi wa habari huko Brasilia, Machi 5, 2021. AFP - EVARISTO SA

Wakati Brazil ikirekodi rekodi mpya za kila siku za vifo kutokana na janga la COVID-19 wiki hii, Rais Jair Bolsonaro metoa wito kwa raia wake kuacha "kunung'unika" na kusonga mbele, huku akikosoa tena dhidi ya hatua za watu kutokaribiana kwa umbali wa mita kadhaa.

Matangazo ya kibiashara

"Je! Mtakaa nyumbani kwa muda wa kiasi gani na kufungiwa kwa kila kitu? Hakuna mtu anayeweza kuvumilia hili tena. Tunasikitishwa na vifo, narejelea hili, lakini tunahitaji suluhisho," amesema kiongozi huyo wa mrengo wa kulia kwa umati uliokusanyika kwa hafla huko Brasilia Alhamisi wiki hii.

Jair Bolsonaro, ambaye amepuuzia tena hatari ya mgogoro wa kiafya, amesema anasikitisha na hatua za kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo na kukosoa Jumatano tangazo la gavana wa Jimbo la Sao Paulo la kufungwa kwa maduka kuanzia Jumamosi.

Kulingana na takwimu kutoka Wizara ya Afya, maambukizi mapya 75,102 yarekodiwa katika muda wa saa ishirini na nne nchini Brazil, rekodi tangu mwezi Julai mwezi uliyopita, wakati vifo 1,699 vipya vikiripotiwa.

Kwa jumla, karibu maambukizo milioni 10.8 na vifo 260,970 vimerekodiwa tangu kuzuka kwa janga hilo.