Majaji watakaosikiliza kesi dhidi ya mauaji ya George Floyd watajwa
Imechapishwa: Imehaririwa:
Majaji watatu mpaka sasa watakaosikiliza kesi ya mauaji dhidi ya Mmarekani mweusi George Floyd, aliyepoteza maisha baada ya kuuliwa na polisi mzungu Derek Chauvin wameteuliwa.
Polisi huyo aliyekuwa anafanya kazi katika kituo cha polisi mjini Mennepolis, anatuhumiwa kumuua Floyd mwaka 2020 kwa kumwekea goti shingoni mpaka akapoteeza maisha.
Kesi hiyo ambayo ilikuwa imepangwa kuanza siku ya Jumatatu, sasa inatarajiwa kuendelea baada ya Majaji kuanza kupatikana na sasa hatima ya polisi huyo ipo mikononi mwa mwao.
Hata hivyo, kesi yenye inatarajiwa kuanza tarahe 29 mwezi huu baada ya mchakato wote wa kuwatafuta mashahidi wa upande wa mashataka na utetezi kukamilika.
Mauaji ya George Floyd yalizua maandamano makubwa nchini Marekani, na kurejesha historia mbaya ya ubaguzi wa rangi nchini Marekani, na Wamarekani weusi wanatumai kuwa haki itatendeka.