MAREKANI-COVID 19

Mswada wa kuwasaidia Wamerekani walioathiriwa na Covid 19 wapitishwa

Bunge la wawakilishi nchini Marekani
Bunge la wawakilishi nchini Marekani Eric BARADAT AFP

Bunge la Congress nchini Marekani, limepitisha mswada wa Dola Trilioni 1 nukta 9 uliokuwa umependekezwa na rais Joe Biden, kuwasaidia Wamerekani ambao wameathiriwa zaidi na Janga la Covid 19.

Matangazo ya kibiashara

Mswada huo uliungwa mkono na wawakilishi wote kutoka chama cha Democratic huku wale wa Republican wakiupinga.

Rais Biden sasa anatarajiwa kuutia saini siku ya Ijumaa, kwa ,mujibu wa msemaji wa Ikulu Jen Psaki.

Naweza kuwatibitishia kuwa rais atautia  saini mswada huu siku ya Ijumaa katika Ikulu ya Marekani, tumekuwa tukipambana kwa siku kadhaa sasa kuhakikisha kuwa mswada huo unakamilika na sasa baada ya kupitishwa taratibu zingine zitafutwa na rais atakuwa tayari kuutia saini siku ya Ijumma.

Mswada huo unaeleza kuwa Wamarekani walio wengi walioathiriwa na mamabukizi ya Corona, watalipwa Dola 1,400.

Watu waliopoteza ajira kutokana na janga la Corona nchini humo, watalipwa Dola 300 hadi mwezi Septemba.

Aidha, imependekezwa kuwa mshahara wa chini kwa wafanyikazi nchini humo, kimeongezwa kutoka Dola 7.25 kwa saa moja hadi Dola 15.